Ezra Chiloba abanduliwa kutoka mamlaka ya mawasiliano

  • | Citizen TV
    4,534 views

    Kusimamishwa kazi kwa muda kwa mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya mawasiliano Ezra Chiloba na bodi ya mamlaka hiyo kumebua masuali si haba, wengi wakitaka kujua sababu za bodi hiyo kuchukua hatua hiyo bila kuweka wazi yaliyojiri. Hata hivyo stakabadhi zilizochipuka zinaratibu matokeo ya mikutano kadhaa ambayo mwishowe yalimweka chiloba na maafisa wengine katika mamlaka hiyo motoni.