Familia moja katika kijiji cha Oterit, huko Mogotio kaunti ya Baringo iliandaa sherehe ya kufana ya kuadhimisha miaka 96 ya nyanya yao, Teriki Sogomo. Sherehe hiyo ya kufana iliwaleta pamoja jamaa, majirani na washirika wa kanisa ambao waliimba, walicheza densi na kushiriki maombi kabla ya kukata keki kwa heshima ya nyanya huyo waliyemtaja kuwa nguzo muhimu na mtu mwenye busara. Katika hafla hiyo wito ulitolewa kwa watoto na jamii kwa jumla kuwahudumia wazazi wao wazee.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive