Familia Kakamega inaomboleza kifo cha bibi harusi aliyefariki kwenye ajali ya barabarani

  • | Citizen TV
    2,499 views

    Familia na marafiki wa bibi harusi aliyekuwa kati ya watu watano waliofariki kwenye ajali barabara ya Turbo - kwenda Webuye wameanza mipango ya mazishi. Jamaa za Brenda Mashekwe wa miaka 29 wanaomboleza kifo chake kijiji cha Ebulechia kaunti ya Kakamega. Marehemu alikuwa akisafiri kwenye gari moja na watu wengine saba waliokuja nyumbani kwao kwa mazungumzo ya mahari. Jamaa zake wakieleza namna ajali hiyo ilitokea baada ya furaha ya ndoa yake