Familia kudai haki ya jamaa yao aliyejeruhiwa na majambazi

  • | Citizen TV
    497 views

    Familia moja katika eneo la Mau Narok katika kaunti ya Nakuru inadai haki kwa jamaa wao aliyeponea kifo katika kisa cha wizi wa kimabavu . Joseph Mpoe aliponea chupuchupu baada ya kufyatuliwa risasi na genge la watu lililozuia gari walilokuwa wakisafiria katika eneo la Soilo katika barabara kuu ya Nakuru kuelekea Kisumu. Washukiwa saba walifikishwa mahakamani kwa kosa la mauaji japo waliachiliwa kutokana na ukosefu wa ushahidi wa kutosha.