Familia moja eneo la Mwala inalilia haki baada ya mwanao kufariki akiwa ndani ya seli

  • | Citizen TV
    1,433 views

    Familia moja katika eneo la Mwala kaunti ya Machakos inalilia haki baada ya mwanao kudaiwa kufariki akiwa mikononi mwa polisi. Familia hiyo inadai mpendwa wao alifariki alipokuwa akizuiliwa katika kituo cha polisi cha makutano. Familia hiyo inasema mwanao alikamatwa na polisi na kuwajulisha kuhusu tukio hilo. Siku nne baadaye walipata ripoti kutoka kwa polisi kuwa alikuwa amejitia kitanzi na kuwa polisi walimpata akiwa sakafuni.