KILIO CHA FAMILIA
Familia moja katika kijiji cha Shinoyi, eneo bunge la Navakholo, kaunti ya Kakamega imetoa wito kwa serikali ingilie kati kuhusiana na mzozo uliopo baina yao na polisi. Familia hiyo imedai polisi wamewanyima idhini ya mazishi ambayo inahitajika ili waweze kumzika mwanao wa kiume mwenye umri wa miaka -17. Mwanafunzi huyo anayefahamika kama Oliver Makoha, aliripotiwa kuuawa akiwa anaelekea kwenye sherehe ya maombolezi almaarufu disco Matanga. Familia hiyo sasa inadai maafisa wa usalama katika eneo hilo wanahujumu juhudi zao za kutaka kumzika mpendwa wao, huku ikitoa wito kwa asasi husika ziingilie kati ili haki itendeke.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive