Familia na jamaa wafanya kumbukumbu ya Erickson Mutisya

  • | Citizen TV
    225 views

    Mwaka mmoja baada ya Erickson Mutisya kuuawa kwa kupigwa risasi na polisi wakati wa maandamano ya kupinga Mswada wa Fedha wa mwaka 2024, familia yake inasema haijapata haki wala aina yoyote ya fidia kutoka kwa serikali. Walipokuwa wakiadhimisha kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kifo chake, hisia zilitanda nyumbani kwa familia hiyo, ambako majirani, marafiki na jamaa walikusanyika kumuenzi kijana huyo na kutoa wito kwa serikali kuacha kuwaua vijana.