- 1,205 viewsFamilia ya Sheila Jepkorir Chebii, Mkenya aliyefariki ughaibuni katika njia tata, inataka Wizara ya Masuala ya Kigeni kuwapa majibu kuhusu kifo cha mwana wao wiki chache tu baada ya kutua nchini Australia. Chebii aliripotiwa kupatikana amefariki katika hoteli moja mjini Sydney mwezi uliopita, polisi nchini humo wakisema alijitoa uhai kwa kujirusha kutoka ghorofa ya 19. Familia hiyo aidha imetilia shaka ripoti hiyo na kutaka ubalozi wa Kenya nchini Australia uchunguze kifo hicho.