- 967 viewsDuration: 2:48Familia ya marehemu Silvester Peter Mwenda ambaye anadaiwa kufariki mikononi mwa maafisa wa Polisi waliyemkamata Ijumaa iliopita inalilia haki. Mwili wa Marehemu Mwenda ulipatikana katika makafani ya hospitali ya Nyambene Level 4 kaunti ya Meru, siku moja baada ya kutoweka nyumbani kwake eneo la Kiina, Igembe Kazkazini.