- 758 viewsDuration: 2:30Familia moja kutoka Timboroa kaunti ya Baringo inaitaka serikali kuwasaida kupata mwili wa jamaa yao aliyeaga dunia katika vita kati ya Urusi na Ukraine. Kevin Kang’u, anadaiwa kupata ufadhili wa elimu nchini Urusi, ila alitakiwa kujiunga na jeshi la taifa hilo kwa mwaka mmoja kabla ya masomo. Na kama anavyoarifu Laura Otieno, ombi hili linajiri siku moja baada ya ubalozi wa Urusi nchini kukana madai ya kuwahadaa baadhi ya Wakenya na kuwatuma katika vita hivyo