Skip to main content
Skip to main content

Familia yataka majibu kufuatia kifo cha polisi Kabiru nchini Haiti

  • | Citizen TV
    2,396 views
    Duration: 3:02
    Familia ya Benedict Kabiru, afisa wa polisi aliyeripotiwa kutoweka wakati wa operesheni ya kiusalama nchini haiti mwezi machi mwaka huu sasa inataka majibu kamili kutoka kwa serikali kufuatia kauli ya rais william ruto hapo jana kuwa alifariki. Katika kikao maalum cha kujadili oparesheni inayoendelea haiti huko marekani, rais ruto aliwaomboleza maafisa watatu akiwemo kabiru ambaye familia yake imekuwa ikiarifiwa kuwa bado anasakwa. Familia hiyo ilielekea mahakamani kutaka serikali ishurutishwe kutoa taarifa kamili huku ikitaka mwili wa marehemu urejeshwa nchini.