Familia za waathiriwa wa Shakahola zataka zipewe miili ya wapendwa

  • | Citizen TV
    346 views

    Familia ambazo miili ya jamaa zao ilitolewa katika msitu wa Shakahola sasa zinataka serikali kuwapa miili hiyo kwa shughuli za mazishi. Baadhi ya jamaa za waathiriwa wakisema kuwa kimya cha serikali kuhusu matokeo ya sampuli za msimbojeni wa DNA zilizochukuliwa mwezi Mei kimewaacha njia panda. Wanaharakati wa haki pia wanaitaka idara ya ujasusi kutoa matokeo hayo ili kuanzisha mchakato wa kupata haki kwa waathiriwa wa sakata hii ya dini potofu iliyoongozwa na Paul Mackenzie