FIFA yaiondolea Kenya marufuku

  • | Citizen TV
    224 views

    Shirikisho la soka duniani FIFA linatarajiwa kutuma ujumbe wake na ule wa CAF kutathmini hali ya soka nchini baada ya kutangaza kuondoa marufuku yake ya muda kwa Kenya. Kulingana na barua iliyotiwa saini na katibu mkuu wa FIFA Fatma Samoura, ujumbe huo pia utakutana na waziri wa michezo Ababu Namwamba. Kenya imepata nafuu hiyo baada ya kufunguliwa kwa afisi za FKF sawa na kurudishwa afisini kwa maafisa wa FKF.