FKE: zaidi ya watu 70,000 wamepoteza kazi kwa mwaka mmoja

  • | Citizen TV
    1,552 views

    Mwaka wa 2023 ulishuhudia dhiki ya ukosefu wa ajira, haswa miongoni mwa vijana. Maelfu ya wakenya wasiokuwa na ajira wamekuwa wakifurika katika kampuni mbalimbali zinapotangaza nafasi za kazi bila mafanikio. Kulingana na takwimu za idara ya takwimu ya kitaifa, KNBS, vijana milioni 4.5 hawana kazi. Rais William Ruto amesema serikali inafanya kila juhudi kuhakikisha inabuni nafasi za ajira kupitia mipango kama ujenzi wa nyumba za bei nafuu. Gatete Njoroge anaangazia hali ya ukosefu wa ajira nchini.