Gachagua Aikosoa Kenya Kwanza, Aahidi Mabadiliko Kabla ya Uchaguzi wa 2027

  • | K24 Video
    1,474 views

    Kiongozi wa chama cha demokrasia ya wananchi, Rigathi Gachagua, ameonyesha kutoridhika kwake na uongozi wa sasa wa Kenya Kwanza, akiwashtumu viongozi wa muungano huo kwa kupuuza matatizo halisi yanayowakumba wananchi huku wakiendelea kumsifu Rais William Ruto. Akihutubia wakazi wa Dagoretti, eneo bunge la Kikuyu, Gachagua aliahidi kuleta mabadiliko kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027, akisema wananchi wanaendelea kutaabika kutokana na gharama ya juu ya maisha pamoja na huduma duni katika sekta za afya na elimu