- 8,638 viewsDuration: 2:30Kinara wa DCP Rigathi Gachagua ameendelea kumshambulia Waziri wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen, akisema ameshindwa kukabiliana na wahuni. Gachagua sasa anatishia kuwa Wakenya watajilinda ikiwa visa vya uhuni vitaendelea. Akizungumza huko Kirinyaga, Gachagua pia aliendelea kujipiga kifua baada ya ushindi wa uchaguzi mdogo wa Ol-Kalou, akisema sasa anaanza safari ya kuunganisha Mlima Kenya. Emmanuel Too anaarifu.