Skip to main content
Skip to main content

Gachagua amtetea Uhuru, akosoa siasa za chuki

  • | Citizen TV
    840 views
    Kinara wa chama cha DCP Rigathi Gachagua amemtetea Rais mstaafu Uhuru Kenyatta akisema kuwa kustaafu kwake hakumaanishi kwamba hafai kuzungumzia masuala ya kitaifa. Akizungumza katika Kaunti ya Nakuru County alipohudhuria ibada ya wafu, Gachagua aliwataka viongozi wa chama cha UDA kukoma kumshambulia Uhuru ili kuficha kile alichokitaja kama utendaji duni wa serikali. Pia amewakosoa wanasiasa wanaoeneza siasa za chuki na ukabila, akionya kuwa matamshi yao yanahatarisha usalama wa kitaifa.