Gachagua asema amechanganyikiwa na ameshindwa na Kazi

  • | Citizen TV
    2,247 views

    Aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua amepuuzilia mbali matamshi ya Rais William ruto ambaye anawalaumu wazazi, makanisa, mashirika ya kijamii na wanasiasa kwa kuchochea maandamano ya kupinga serikali. Gachagua anadai kuwa Rais Ruto amechanganyikiwa kuhusu yanayoendelea nchini. Akizungumza mjini Dracut, Massachusetts nchini Marekani, Gachagua aliendeleza kampeni ya kumtaka Rais Ruto kuondolewa mamlakani mwaka wa 2027, akiwaambia wakenya wanaoishi mjini humo kuwa Rais Ruto ameshindwa na kazi