Gachagua asema upinzani kumshtaki Ruto ICC

  • | Citizen TV
    9,910 views

    Kinara wa Chama cha DCP Rigathi Gachagua sasa anadai kwamba Mawakili wa upinzani wanakusanya ushahidi ili kumshtaki Rais William Ruto Katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa jinai -ICC- kuhusiana na umwagikaji wa Damu na mauaji Nchini. Gachagua anadai kwamba Ruto amekiuka kiapo alichochukua alipopishwa kama rais cha kuchunga maisha na mali ya wakenya kwa kutoa amri kuwa wakenya wapigwe risasi.