Gachagua: Azimio watarudishiwa ulinzi baada ya miezi 3

  • | Citizen TV
    9,411 views

    Viongozi wa Azimio waliopokonywa walinzi watarejeshewa walinzi hao baada ya miezi mitatu. Hayo ni kwa mujibu wa naibu rais Rigathi Gachagua ambaye amesema kuwa hatua hiyo itachukuliwa pale upinzani utakapositisha maandamano. Gachagua amesema polisi waliokuwa wakiwalinda viongozi wa azimio wana majukumu ya kuwakabili waandamanaji. Na kama anavyoarifu Gatete Njoroge, Gachagua amewaonya wapinzani dhidi ya kufanya maandamano akisema polisi watakabiliana nao vilivyo.