Gavana Dhadho Godhana ataka serikali kusaidia familia zilizoatharika na mafuriko

  • | Citizen TV
    197 views

    Gavana wa Tana River Dhadho Godhana ametoa wito kwa serikali ya kitaifa na mashirika ya kibinadamu kujitokeza na kusaidia familia zilizoatharika na mafuriko katika kaunti hiyo. Akizungumza katika makao makuu ya shirika la Msalaba Mwekundu eneo la Hola, Godhana amesema kuwa familia nyingi zilipoteza mali zao katika mafuriko yaliyosababishwa na mvua za El Nino. Aidha familia hizo zimekuwa zikitegemea misaada kukidhi mahitaji yao lakini serikali ya kaunti imelemazwa na juhudi za kutua misaada kwa waathiriwa hao.