Gavana wa kaunti ya kwale Kwale Fatuma Achani amefanya mazungumzo na vijana walioasi uhalifu kutoka huko diani pamoja na idara ya usalama eneo la Msambweni.
Mkutano huo unajiri wakati vijana kutoka maeneo ya Tiwi,Kombani , Diani Waa na Ng'ombeni wamekuwa wakihangaisha wakazi kwa kuwavamia na kuwaibia. Akizungumza wakati wa mkutano huo katika ukumbi wa mikutano wa Mvindeni, huko ukunda Gavana Achani amewataka vijana wa kaunti ya Kwale kutojihusisha na visa vya utovu wa usalama kwani vimeathiri pakubwa sekta ya utalii na uwekezaji .