- 495 viewsDuration: 1:38Gavana wa Siaya James Orengo anasema chama cha ODM hakitamuunga mkono rais William Ruto katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2027 akisema kuwa chama cha UDA ndicho kinapaswa kuunga mkono ODM. Kulingana naye, kwa vile ODM kina umaarufu zaidi ya vyama vyote nchini, hakiwezi kuwa chini ya chama kingine. Orengo alikuwa akizungumza alipoitembelea familia ya mbunge wa zamani wa Lugari marehemu Cyrus Jirongo pamoja na viongozi wengine nyumbani kwa mwendazake Lugari.