- 1,142 viewsMahakama kuu imempa afueni gavana wa kaunti ya Isiolo Abdi Guyo baada ya majaji kutupilia mbali kesi iliyowasilishwa ikitaka abanduliwa Ofisini. Kwenye kesi hiyo, Guyo na naibu wake John Lowasa, walitakiwa kujiuzulu kutokana na madai kwamba walihama kutoka chama cha Jubilee walichotumia kugombea viti na kujiunga na chama cha UDA. Majaji walitupilia mbali kesi hiyo kwa msingi kwamba hakukuwa na ushahidi wa kutosha wa kudhibitisha kuwa wawili hao walijiuzulu rasmi kutoka Jubilee.