Gavana wa Uasin Gishu akana serikali yake imeshindwa kuwalipia gharama ya wanafunzi walioko Finland

  • | Citizen TV
    1,369 views

    Gavana wa Uasin Gishu Jonathan Bii amekana ripoti kuwa serikali ya kaunti hiyo imeshindwa kulipia gharama za wanafunzi walioelekea nchini Finland kwa masomo. Gavana Bii sasa akisema kuwa serikali ya kaunti hiyo haikuwa inafadhili elimu ya wanafunzi hao japo ilikuwa tu inawasaidia wazazi kufanikisha stakabadhi za usafiri. Na kama Serfine Achieng Ouma anavyoaripoti, Familia za wanafunzi walio kwenye hatari ya kufurushwa zikitaka hatua za dharura kuchukuliwa