Geoffrey Chesoni, mwanablogu aliyetekwa nyara na polisi Mombasa aeleza mateso aliyopitia

  • | Citizen TV
    9,018 views

    Mwanablogu aliyetekwa nyara Jumanne katikati ya jiji la Mombasa amesimulia kichapo alichopitia mikononi mwa maafisa wa polisi kwa siku tatu. Geoffrey Chesoni anadai kusafirishwa hadi msituni huko Voi na kuchapwa, kutishiwa maisha na maafisa saba kabla ya kuletwa ikulu ya Mombasa na kutibiwa na kisha kuwachiliwa. Na kama anavyoarifu Francis Mtalaki, Chesoni anahofia maisha yake.