Gharama ya mishahara yahujumu maendeleo

  • | Citizen TV
    48 views

    Serikali inapania kupunguza mzigo wa mishahara ya wafanyikazi ili kuafikia silimia 35 ya mapato. Kwenye kongamano la kitaifa kuhusu mishahara lililowaleta pamoja maafisa wakuu wa serikali kuu na za kaunti, mwenyekiti wa tume ya mishahara Lyn Mengich amelalamikia gharama ya mishahara akisema kuwa inachukua zaidi ya asilimia 40 , hali ambayo inasababisha miradi ya maendeleo kuathirika.