Gor kuchuana na Nairobi United Jumapili uwanjani Ulinzi

  • | Citizen TV
    205 views

    Timu ya Gor Mahia imekamilisha maandalizi yake ya fainali ya mchuano wa FKF dhidi ya Nairobi United Jumapili hii uwanjani ulinzi complex. Gor ambao walikosa taji la ligi kuu nchini kwa maafisa wa Police FC, wameahidi kujitolea asilimia mia moja ili kunyakuwa taji hilo. Wanachuana na Nairobi United walioshinda ligi ya NSL na kupandishwa daraja hadi ligi kuu kuelekea msimu ujao. Mshindi wa fainali hiyo atawakilisha Kenya katika mchuano wa mashirikisho barani Afrika msimu ujao.