- 696 viewsNi mzee mwenye umri wa miaka 86 lakini amepata umaarufu mkubwa katika kaunti ya Lamu kutokana na ujuzi wake wa kupiga mbizi na kuokoa maisha na mali baharini. Tunamzungumzia Mzee Ali Suo Bakari, ambaye amekuwa akipiga mbizi kwa zaidi ya miaka 60. Abdulrahman Hassan aliandamana na mzee huyo baharini na kuangazia safari yake ya mwisho huku akijiandaa kustaafu kutokana na kudhoofika kwa afya yake.