Hamas ni nini?

  • | VOA Swahili
    251 views
    Hamas, ni kifupi cha Harakat al-Muqawama al-Islamiya (“Kikundi cha Harakati za Kujihami cha Kiislam”), kilichoanzishwa na Sheikh Ahmed Yassin, mwanazuoni wa Kipalestina. Ni harakati za wanamgambo na moja ya vyama vikuu viwili vya kisiasa katika eneo la Palestina. Hamas inawaongoza zaidi ya Wapalestina milioni mbili huko Ukanda wa Gaza, lakini kikundi hicho ni maarufu zaidi kwa operesheni zake za silaha dhidi ya Israeli. Darzeni ya nchi zimeitaja Hamas ni taasisi ya kigaidi, ijapokuwa baadhi kitengo chake cha kijeshi ni cha wanamgambo. Mnamo mwaka 1997, Marekani ilikitaja kikundi cha Hamas kuwa taasisi ya kigeni ya kigaidi. Wapalestina wana eneo dogo la kujitawala huko Ukingo wa Magharibi na wamegawanyika kati ya utawala unaoungwa mkono na Magharibi na Kikundi cha Kiislam cha Hamas chenye silaha ambacho kinakataa kuishi pamoja na Waisraeli. Hivi leo, Iran inaaminika kuwa moja ya wafadhili wakubwa kabisa wa Hamas, wakichangia fedha, silaha na mafunzo. #israel #gaza #reels #igreels #videography #voa #hamas