Zoezi la uhamasishaji na upimaji wa Virusi vya UKIMWI (HIV) limeandaliwa katika mji wa Nanyuki, likiwakusanya vijana kwa lengo la kuwahimiza kujitokeza kujua hali zao za afya na kuchukua hatua stahiki mapema.
Mpango huo ulilenga kuongeza uelewa kuhusu kinga, matibabu na umuhimu wa kupimmwa mara kwa mara. Katika shughuli hiyo, vijana walipata huduma ya upimaji wa HIV kwa hiari pamoja na ushauri nasaha kutoka kwa wahudumu wa afya huku waandalizi wakisema bado kuna hofu na taarifa potofu miongoni mwa vijana zinazowazuia kujitokeza kupimwa.