- 3,050 viewsDuration: 3:43Mtanzania Shedrack Chaula, hajulikani alipo kwa mwaka mmoja sasa, familia yake imekuwa ikumtafuta katika maeneo tofauti tofauti bila mafanikio. Inadaiwa alitekwa siku chache baada ya kuachiwa huru baada ya kukutwa na hatia ya kutenda kosa la kimtandao. Shedrack ambaye ni msanii na mtayarishaji wa maudhui mtandaoni alihukumiwa kifungo au kulipa faini baada ya kusambaza video kupitia mtandao wa kijamii wa TikTok ikionekana akichoma picha ya Rais. Watetezi wa haki wameeleza kuwa wanaharakati na wanasiasa wa upinzani wanapotea. Serikali ya Tanzania imekanusha kuhusika na matukio ya watu kupotea. BBC ilituma maombi ya mahojiano na polisi lakini haikujibiwa. Taarifa imeandaliwa na Alfred Lasteck. - - #bbcswahili #utekaji #simanzi Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw