Havi ataka majaji wa mahakama ya upeo waondolewe ofisini

  • | KBC Video
    61 views

    Aliyekuwa rais wa chama cha wanasheria nchini, Nelson Havi, anataka jopo la majaji watatu lililobuniwa kusikiza rufaa ya kumwondoa jaji mkuu Martha Koome na majaji wengine sita wa mahakama ya upeo livunjwe. Kupitia hati ya dharura Havi ametoa sababu nyingi kuhusiana na rufaa yake akitaka jopo jipya liteuliwe. Jopo hilo la majaji watatu linalowajumuisha majaji Charles Kariuki, Lawrence Mugambi, na Bahati Mwamuye pia lilikabiliwa na kipindi kigumu kuelezea ni kwa nini swala linalmhusu jaji mkuu lilitengewa kusikizwa mwezi oktoba badala ya mapema zaidi. Majaji hayo wa mahakama ya upeo wanashtumiwa kwa kukiuka katiba na kanuni za maadili za idara ya mahakama.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive