Skip to main content
Skip to main content

Hofu ya mikoko Mombasa

  • | Citizen TV
    46 views
    Wanaharakati kaunti ya Mombasa wameelezea wasiwasi wao kuhusu kupungua kwa mikoko kando ya bahari. Wakizungumza wakati wa zoezi la kupanda mikoko katika mkondo wa bahari eneo la Tudor wametaka wanafunzi shuleni kushirikishwa katika hamasiho la mazingira. Wakaazi wanaofanya uvuvi hilo wamelalamikia kupungua kwa samaki na uchafuzi wa mazingira wanaosema makazi yalioko yamekuwa yakipeleka maji taka baharini. Maafisa wa KWS kwa upande wao wamesema wataendelea na kampeni ya kuhakikisha vijana na watoto wamehusishwa katika utunzaji wa mikoko na mazingira.