- 212 viewsDuration: 1:38Utafiti uliofanywa na madaktari na wataalamu wa ugonjwa wa macho kaunti ya Mombasa umebaini ukosefu wa huduma za afya mapema umechangia kwa kuongezeka kwa ugonjwa huo miongoni mwa umma. Wakiongea huko Mjambere eneo bunge la Kisauni katika hamasisho la kutoa matibabu ugonjwa wa macho umekuwa tishio hasa eneo la Jomvu ambapo idadi kubwa ya wakaazi wanaugua ugonjwa huo hasa umri wa makamu. Madaktari hao wanapendekeza kupunguzwa kwa gharama ya matibabu wakisema inachangia kwa ongezeko la ugonjwa wa macho.