- 3,322 viewsDuration: 2:35Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko makubwa yaliyoshuhudiwa nchini Ijumaa jioni imefikia watu 43. Shirika la msalaba mwekundu likiripoti idadi hii huku mvua kubwa ikiendelea kusababisha uharibifu katika maeneo kadhaa nchini. Katika baadhi ya maeneo ya hapa jijini nairobi, nyumba zimeharibiwa na miundombinu muhimu kuharibika, huku mamia ya familia zikiwachwa bila makao.