Idara ya afya katika kaunti ya Migori yaangazia ongezeko la mimba za mapema eneo hilo

  • | Citizen TV
    151 views

    Idara ya afya katika kaunti ya Migori imeandaa kikao na wadau wa jinsia na wasichana kwa lengo la kutathmini hatua ambazo zimepigwa kumaliza mimba za utotoni katika kipindi cha miaka mitano kaunti hiyo. Takwimu za wizara ya afya zimebaini kuwa hatua kubwa imepigwa kupunguza visa vya mimba za utotoni hadi asilimia 19. Mkurugenzi wa elimu kaunti ya Migori Jacob Onyiego amesema wizara ya elimu imeweka mipango ya usambazaji wa sodo kando na kuhakikisha wasichana waliojifungua wanapata fursa ya kurejea shuleni. Naibu kamishna wa kaunti ya Suna Mashariki Benson Karani ameitaka jamii kutowakinga wahusika wanaowapachika watoto mimba bali wawashtaki ili waweze kuadhibiwa kisheria.