Idara ya mahakama imemulikwa baada ya bunge la kitaifa kuagiza ukaguzi maalum utekelezwe kuhusiana na matumizi ya shilingi bilioni 5.3 za mpango wa nyumba kwa maafisa wa idara hiyo, uliokuwa umetekelezwe nje ya mipaka ya sheria. Akifika mbele ya kamati ya bunge la kitaifa kuhusu uhasibu wa umma (PAC), msajili mkuu wa idara ya mahakama Winfridah Mokaya alikuwa na wakati mgumu kuilezea kamati hiyo jinsi mpango huo wa nyumba kwa maafisa wa idara hiyo umekuwa ukiendeshwa kwa mkataba wa maelewano na benki ya KCB kwa kipindi cha miaka 12 iliyopita bila msingi wa kisheria. Abdiaziz Hashim na maelezo kwa kina.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive