Idara ya usalama Kakamega yaanza mpango wa kurekodi mikutano

  • | Citizen TV
    287 views

    Idara ya usalama kaunti ya kakamega imezindua utumizi wa mtambo wa elektroniki utakaosaidia kuwanasa wanasiasa ambao wataeneza semi za chuki miongoni mwa wapiga kura msimu huu wa kampeni. Akizungumza na wanahabari kabla ya kuanza rasmi zoezi la mbio za amani za kilomita saba mjini kakamega,kamishna wa kaunti ya kakamega john ondego, amewataka wanasiasa kueneza jumbe za amani na kutowatumia vijana kwa kuwapa mihadarati ili kuzua vurugu. Kwa upande wake mkuu wa polisi kaunti hiyo Joseph kigen, amewaonya wanasiasa dhidi ya kutumia vijana kuvuruga amani huku akiwataka kutumia fursa hiyo kueneza amani miongoni mwa wananchi.