IEBC kunadi mali ya wanasiasa walio na madeni yake

  • | KBC Video
    56 views

    Tume huru ya uchaguzi na mipaka ,IEBC sasa inatafuta huduma ya madalali kuwasaka wanasiasa ,walalamishi na kampuni nyingine kadhaa kwa kushindwa kulipa tume hiyo ,jumla ya shilingi million 400 kuambatana na maagizo ya mahakama.Akiongea alipofika mbele ya kamati ya bunge kuhusu uhasibu wa pesa za umma,afisa mkuu mtendaji wa tume hiyo Hussein Marjan amesema baadhi ya watu waliopoteza kesi za kupinga matokeo ya uchaguzi dhidi ya tume hiyo, na kuagizwa na mahakama kugharamia kesi hizo ,wametafuta huduma ya mawakili wakijaribu kukwepa kulipa pesa tume hiyo inawadai.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive