Skip to main content
Skip to main content

IEBC yamteua Moses Ledama Sunkuli kuwa kaimu afisa mkuu wa tume hiyo

  • | Citizen TV
    189 views
    Tume huru ya uchaguzi na Mipaka IEBC ilimteua Moses Ledama Sunkuli kuwa kaimu Afisa Mkuu wa tume hiyo kwa muda wa miezi 6. Ledama Sunkuli mwenye tajriba ya miaka 12 kwenye masuala ya uchaguzi anachukua mahala pake Marjan Hussein Marjan ambaye aliondoka siku mbili zilizopita.Mwenyekiti wa tume hiyo Erastus Ethekon amesema kuwa Sunkuli atashikilia wadhifa huo hadi pale Afisa Mkuu atakapoteuliwa kikamilifu. Na kama anavyoarifu Seth Olale, uteuzi wa Sunkuli ni mojawapo ya mabadiliko yanayofanyiwa IEBC huku mchakato wa maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2027 ukishika kasi.