- 284 viewsTume ya uchaguzi nchini IEBC imepuuzilia mbali matamshi kuhusu madai ya wizi wa kura katika uchaguzi mkuu ujao, huku ikiwaonya wanasiasa wanaoeneza uvumi huo. Mwenyekiti wa IEBC Erustus Ethekon amesema kuwa matamshi hayo yanahujumu juhudi za tume hiyo za kuandaa uchaguzi mkuu ulio huru na wa haki. Tume hiyo imesisitiza kuwa inaendelea na maandalizi kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa kuaminika na wa uwazi.