IEBC yasema hakutakuwa na sajili ya wapigakura iliyochapishwa

  • | Citizen TV
    2,187 views

    Uchaguzi mkuu wa mwaka huu utaandaliwa bila kuwepo kwa sajili ya wapigakura iliyochapishwa. Tume ya uchaguzi nchini IEBC inasema uamuzi huo uliafikiwa baada ya tathmini ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2017 na marudio ya uchaguzi wa urais kuonyesha kuwa sajili hiyo inaweza kutumiwa visivyo. Haya yamefichuliwa kwenye taarifa ya tume ya uchaguzi IEBC ya kujibu maswali 9 yaliyobuliwa na muungano wa Azimio