- 4,204 viewsDuration: 3:25Imamu Omar Athman aliyehusishwa na ulaghai wa safari za wakenya kwenda Hajj nchini Saudi Arabia atajua hatma ya endapo ataachiliwa au la hapo kesho. Imam Omar alifikishwa mahakamani kwa madai ya ulaghai wa zaidi ya shilingi laki saba katika mpango wa kuandaa safari ya kwenda kuhiji Mecca. Kufuatia kukamatwa kwake, waathiriwa wengine wanaodai kulaghaiwa wamejitokeza katika vituo mbalimbali vya polisi kurekodi taarifa.