Jaji Mkuu atetea uwajibikaji na uhuru wa mahakama

  • | Citizen TV
    1,615 views

    Jaji Mkuu Martha Koome ametoa hakikisho kuwa mkutano kati yake na Rais William Ruto hauwezi kuathiri kwa vyovyote uhuru wa idara ya mahakama. Akizungumza katika mkutano na majaji na viongozi wa mahakama uliofanywa kudadisi hatua walizopiga kufanikisha utendakazi wao, Jaji Mkuu alisema ushirikiano na ofisi nyingine za serikali ulikuwa wa kuhakikisha masuala yanayotatiza utendakazi wa idara ya mahakama yanashughuliwa. Hata hivyo, Koome kwenye taarifa yake ameonya dhidi ya mazungumzo yoyote ambayo huenda yakaathiri maamuzi ya kesi akisema kuwa hilo halitakubaliwa. Koome pia akisema uchunguzi zaidi unafaa kufanywa kutathmini iwapo kuna njia ya kuhakikisha kesi zinazohusu umma na zinazositisha kwa muda mipango ya serikali zinakamilishwa haraka ili kupunguza lawama kwa mahakama.