Skip to main content
Skip to main content

Jamaa za mwanamke anayedaiwa kubakwa yalalama Bomet

  • | Citizen TV
    396 views
    Familia moja kutoka Chemaner kaunti ya Bomet inalilia haki baada ya mwanawao mjauzito kuripotiwa kubakwa katika hospitali ndogo ya Chemaner na mhudumu wa hospitali hiyo. Familia inasema kuwa hawajafurahishwa na jinsi kesi hiyo inavyoendelea na hawana imani iwapo mwanawao atapata haki wakisema mshukiwa amejaribu mara kadhaa kuingilia uchunguzi. Wakati uo huo wanaharakati wa kutetea dhulumu za kijinsia katika kaunti ya Bomet wanataka idara ya polisi kushughulikia kesi hiyo ili mwathiriwa apate haki.