Jamii ya Endorois imepata ushindi mkubwa wa kihistoria katika kesi dhidi ya Serikali kuhusu kutangazwa kwa eneo kubwa la Arabal katika Kaunti ya Baringo kuwa ardhi ya msitu,uamuzi ambao pia unaathiri ardhi inayohifadhi Shule ya Msingi ya Loromoru, iliyobomolewa na Huduma ya Misitu Kenya (KFS) mwezi uliopita.
Katika uamuzi uliotolewa na Jaji Millicent Odeny wa Mahakama ya Mazingira na Ardhi ya Nakuru, mahakama ilibaini kuwa mchakato uliopelekea kutangazwa kwa eneo la Arabal kuwa msitu ulikuwa kinyume cha katiba na sheria kwa kukosa ushirikishwaji wa umma unaotakiwa kisheria.