Skip to main content
Skip to main content

Je Kenya inapaswa kuwa na wasiwasi kiusalama kuelekea uchaguzi 2027?

  • | BBC Swahili
    5,199 views
    Duration: 2:58
    Leo Alhamisi Julai 16, wapiga kura takriban 72,997 wanashiriki katika uchaguzi mdogo kuchaguwa muwakilishi wao katika bunge la kitaifa nchini Kenya baada ya kufariki kwa aliyekuwa mbunge wa eneo hilo David Njuguna Kiaraho. Na huku wengi haswa nchini Kenya wakifuatilia uchaguzi huo mdogo unaofanyika mwaka mmoja kabla ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027, matukio ya ghasia yaliyoshuhudiwa wakati wa kampeni zimetia doah shughuli hiyo ya kikatiba kwasababu ya suala la uhuni unaofanyika wazi, mchana peupe na ambao wengi nchini kenya wanahisi umewashinda maafisa wa usalama kuudhibiti. Swali kuu ni je, kenya inapaswa kuwa na wasiwasi kuhusu hali mbaya ya kiusalama kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027? Mwandishi wa BBC Leila Mohammed @mrs.tadicha na tathmini ya kina. - - #bbcswahili #kenya #uchaguzi #Uongozi Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw