Je kwanini Wanajeshi wa Tanzania wataendelea kusalia nchini Msumbiji?

  • | BBC Swahili
    1,036 views
    Ujumbe wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ambao unajumuisha wanajeshi kutoka nchi nane, umesema utaondoa vikosi vyake kutoka Msumbiji ifikapo Julai 15, kwa kuzingatia mkataba wake wa miaka mitatu. Botswana na Lesotho tayari zimewaondoa wanajeshi wao, huku Angola na Namibia zikiwa katika harakati za kuondoka. Gazeti binafsi la Zambeze la mjini Maputo liliripoti kuwa Tanzania, ambayo inapakana na Msumbiji upande wa kaskazini, itawabakisha mamia ya wanajeshi wake. Je kwanini Tanzania inabakiza wanajeshi wake nchini humo? Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wa Tanzania Stergomena Tax anaelezea #bbcswahili #tanzania #msumbiji Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw