Je, miti ina kumbukumbu?

  • | BBC Swahili
    309 views
    Dk. Estrella Luna-Diez kutoka Chuo Kikuu cha Birmingham amefanya utafiti ili kujua kama miti inaweza kukumbuka changamoto za ukame na baridi kali. Mradi wa MEMBRA wenye makao yake nchini Uingereza huangalia sampuli za majani na mbegu ili kuchunguza kama miti inaweza kupitisha kumbukumbu zozote za msongo wa mawazo hadi kwenye miche yao, na ikiwa kizazi kipya kitakuwa na ustahimilivu zaidi. #bbcswahili #uingereza #utafiti